JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
 
     
  USHIRIKA
 
[ Ushirika ] Programu.. [ Nyumbani ] au
 
Majukumu ya Ofisi ya Ushirika Mkoa

 

 1. Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) juu ya Kujenga uwezo wa Halmashauri mkoani na kuratibu shughuli zote za ushirika katika mkoa hususani:-
  • Kusajiri Vyama vya ushirika.
  • Kukagua vyama vya ushirika.
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu zote za ushirika.
  • Kuvitafutia masoko vyama vya ushirika na kufanya utafiti wa masoko.
 2. Kumsaidia katibu tawala (RAS) kuzisaidia serikali za mitaa kutathimini matatizo na fursa za maendeleo.
 3. Kumsaidia katibu tawala (RAS) kuandaa taarifa yakiifu ya maedeleo na kutoa ripoti.
 4. Kuandaa ripoti ya maendeleo ya ushirika yenye mawanda mapana itakayowasilishwa kwenye kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC).
 5. Kumsaidia katibu tawala (RAS) kutoa mwongozo na ushauri kwa serikali za mitaa na asasi zinginezo.
 6. Kuzisaidi serikali za mitaa kutafuta ufumbuzi wa matatizo na fursa zilizopo kwenye mikakati yao ya maendeleo.
 7. Kuweka mipango ya kuijengea halmashauri yeyote kadri inavyohitajika.
 8. Kutathmini na kusimamia programu za maendeleo a kujenga uwezo kwa Mwezi,Robo,nusu na Mwaka .
 9. Usajiri wa vyama vya ushirika mkoani.
 10. Kusimamia utekelezaji wa sera za serikali kuu kwenye Serikali za mitaa kama ilivyoelekezwa`na katibu tawala wa Mkoa(RAS).
 11. Kutafsiri sera,miongozo na kanuni za ushirika kutoka wizarani na asasi ziginezo.
 12. Kufanya majukumu yaliyokasimiwa kutoka wizara za serikali kuu kama itakavyoelekezwa na katibu Tawala wa Mkoa(RAS).

Mkoa una jumla ya wafanyabiashara zaidi ya 7,000 wa jumla na rejareja. Biashara zinazohusika ni kama vifaa vya ujenzi, madawa ya binadamu na mifugo, mafuta aina ya petroli, mafuta ya kula, masonara, wauza nguo mpya na mitumba, wauza nafaka, matunda na kadhalika.

Idadi ya vyama vya Ushirika:

Sekta ya Ushirika ni muhimu sana kupiga vita umaskini. Mkoa wa Mwanza una jumla ya vyama vya ushirika aina mbali mbali vipatavyo 1029 kwa mchanganuo ufuatao:-

 • Vyama vya mazao (AMCOS)    346;
 • SACCO    592;
 • Uvuvi         26;
 • Walaji          9,
 • Viwanda     10;
 • Huduma     14;
 • Umwagiliaji  7,
 • Vinginevyo 24 na
 • Chama kikuu cha ushirika kimoja cha Nyanza Cooperative Union ( NCU (1984) Ltd.).

Vyama vya mazao(AMCOs) vilivyo vingi si hai kwa sababu NCU(1984) Ltd imedorora kwa takribain miaka mitatu haijanunua Pamba – kutoka kwa wanachama wake (Vyama vya Msingi).

HALI HALISI ILIVYO NDANI YA NCU KWA SASA:

Kwa Takribani Misimu mitatu mfululizo (2005/2006; 2006/2007 na 2007/2008) Union haikuweza kununua Pamba kutokana na vikwazo mbalimbali.NCU (1984) Ltd. inakabiliwa na tatizo la madeni makubwa yaliyosababishwa na viongozi na Menejmenti ambapo jumla ya zaidi ya Tshs.6.8 bilioni Union inadaiwa na (Taasisi, Kampuni na Benki) ilizokuwa inafanya shughuli nazo na vilevile NCU (1984) Ltd kukabiliwa na kesi nyingi zaidi ya (22) ambapo kesi zimefunguliwa Mahakamani na Wadai wanaposhinda kesi hukamata mali za NCU na kuziuza kwa bei ndogo ili mradi tu wapate kile wanachodai.
    Pia Union inadaiwa na wakulima mapunjo ya bei (2004/05) zaidi ya Tshs.300 milioni, wafanyakazi wa NCU (1984) Ltd nao wanadai malimbikizo ya mishahara zaidi ya Tshs.868 milioni.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA MKOA ILI KUNUSURU NCU (1984) LTD:

Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika baada ya kuona matatizo yaliyomo ndani ya NCU kwa mujibu wa sheria ya Ushirika Na.20 ya 2003 :-

 1. Iliteua wajumbe watatu wa Bodi ili kuongeza nguvu ndani ya Bodi ya NCU iliyopo kwani ina udhaifu katika kusimamia shughuli za Union (Bahati mbaya wajumbe hao walipata ajali na kufariki dunia) huko mkoani Singida. Mungu aziweke Roho za marehemu mahala pema Peponi.
 2. Mrajis wa Vyama vya Ushirika ameteua Wataalamu watatu (Meneja Mkuu, Mhasibu Mkuu na Mkaguzi wa ndani ili kuongeza nguvu ndani ya Menejimenti ya NCU ili kusaidia usimamizi wa shughuli za kila siku.

 

 

 
 

HALI YA SACCOS:

Katika kipindi cha Agosti. 2006 hadi Agosti, 2007

 • SACCOS 107 zimesajiriwa.
 • Wanachama wameongezeka kutoka 52,605 hadi 63,016 ongezeko la asilimia 20%.
 • Thamani ya Hisa zimepanda kutoka Tshs.980 milioni hadi Tshs. 1.2 bilioni ongezeko la asilimi 22%.
 • Akiba zimeongezeka kutoka Tshs. 1.5 bilioni hadi 2.1 bilioni sawa na asilimia 40.
 • Amana zilizowekwa zimeongezeka kutoka 136 milioni hadi milioni 429 sawa na asilimia 57%.
 • Mikopo imeongezeka kutoka Tshs.4.9 bilioni na kufikia Tshs.10.005 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 100.42%.
 • Idadi ya wanachama wa SACCOs hadi sasa ni 63,016.

Uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia vikundi na SACCOS:

Uwezeshaji wananchi kiuchumi ni kama ifuatavyo:-

 • Wajasilimali 5576 na vikundi 71 waliokopeshwa kupitia NMB ni Tshs.1.184,396,167.00
 • SACCOS 5 kupitia CRDB – Tshs.644,037,000/=
 • Jumla ya Uwezeshaji kwa mikondo hii miwili ni Tshs.1,828,433,167.00        
Mafanikio ya sekta ya ushirika – mkoa wa mwanza:

mafanikio ya sekta ya ushirika hapa mkoani ni kama ifuatavyo:-

 1. Kumekuwepo na ongezeko la vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) ambapo wananchi wameweza kuhamasishwa na kuvianzisha wenyewe ambapo kati ya 2004/2005 na 2006/2007 vyama vya akiba na Mikopo 255 vipya vimeweza kuanzishwa na kusajiriwa na kuwezesha Mkoa kuwa na jumla ya SACCOs 592.
 2. Idadi ya wanachama imeongezeka katika SACCOS toka wanachama 26,300 mwaka 2004/2005 hadi wanachama 63,397 mwaka 2006/2007.

Matatizo/changamoto zinazokabili sekta ya ushirika:

matatizo ya ushirika mkoani ni kama ifuatavyo:-

 1. Upungufu wa Wataalamu wa ushirika katika sekta ya ushirika unaathiri sana utendaji wa shughuli za kila siku za sekta hii hasa katika ngazi ya Wilaya.
 2. Ukosefu wa mitaji katika vyama vya ushirika hasa vyama vya ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) kunakwamisha maendeleo katika sekta ya ushirika.
 3. Ukosefu wa Elimu ya ushirika na Ujasiliamali kwa Wanachama na Wananchi kunaathiri maendeleo ya sekta ya Ushirika Mkoani.
 4. Uongozi na Menejimenti dhaifu hasa ngazi ya Union kumesababisha vyama vya msingi (MAZAO) kutokununua zao la pamba misimu mitatu mfululizo.

Mikakati ya kukabiliana na changamoto za kukuza Sekta ya Ushirika

kutokana na Changamoto hizo hapo juu, mkoa una mikakati ifuatayo kutatua matatizo hayo:-

 1. Kutoa elimu kuhusu nafasi ya ushirika kama sekta ya Kimkakati katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kujenga Uchumi wa Taifa.
 2. Kuongeza idadi ya wanachama kwa lengo la kupanua mitaji.
 3. Kuongeza viwango vya hisa, viingilio, Amana
 4. Kuhimiza vyama vya msingi vya mazao kuanzisha SACCOS ili kuweza kupata mtaji wa kununulia mazao.

kwa muhtasari tu hali ya Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) ni kama ilivyoonyesha hapa chini:-

 1. Idadi ya SACCOs           -        592
 2. Wanachama                   -        63,016
 3. Mtaji                              -        3,587,775,042.50
 4. Mikopo tolewa                -        10,005,021,916/=
 5. Mikopo rejeshwa            -        5,681,515,756/=
Mikopo bado rejeshwa   -        4,324,011,16
 
 

Jedwali kuonyesha mikakati ya sekta ya ushirika mkoa wa Mwanza miaka mitatu ijayo (2007/2008 – 2009/2010).


NO.

LENGO MAHUSUSI

MIKAKATI

SHUGHULI

1.

Kuongeza idadi ya SACCOS katika ngazi za Wilaya toka SACCOS 592 hadi SACCOS 700 ifikapo 2010.

- Uhamasishaji wa wananchi ili wahiari kuanzisha SACCOs hasa katika ngazi ya Kata.
- Uandikishaji wa SACCOS
Kuunganisha SACCOS ndogo ndogo ili ziwe imara kiuchumi.

-  Kufanya mikutano kwa kushiriki kisha
   viongozi na vikundi vya vijana na
   wanawake, viongozi wa Siasa,
   madhehebu ya dini wafanyabiashara
   wadogowadogo na walioko katika
   maeneo husika
-  Kufanya mikutano Wilayani kwa
   kukutana na viongozi wa wilaya ili
   waweze kuhamasisha Wananchi
   waweze kuanzisha SACCOS Imara
   na Endelevu katika Wilaya husika.

2.

Kuongeza ukaguzi wa vyama vya ushirika toka vyama 40 hadi 1000 ifikapo 2010

- Kutoa mafunzo kwa waweka Hazina/Katibu wa SACCOS ili wajue uandishi wa Vitabu vya Hesabu na Usimamizi.
- Kufanya ukaguzi na kufanya mafunzo kazini

- Kufanya mafunzo ya uandishi
   Vitabu na usimamizi wa fehda.

- Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa vyama vyote wilayani.

- Kufanya mafunzo kazini kwa viongozi wa vyama vya ushirika

3.

Kuongeza idadi ya Vyama vya Ushirika vya wavuvi toka vyama 26 hadi 35 ifikapo 2010.

Kuhamasisha jamii kuanzisha vyama vya Wavuvi.

- Kufanya mikutano na Wavuvi
- Kufanya mafunzo juu ya usimamizi
   wa vyama vya Uvuvi.

4.

Kuhamasisha ujenzi wa Ofisi za Kisasa kwa SACCOs toka Ofisi 80 hadi 400 ifikapo 2010.

- Kuhamasisha wanachama wa SACCOS umuhimu wa kuwa na Ofisi za Kisasa za SACCOS.
-Kuziunganisha (Interlinking) SACCOS na Taasisi zingine za kifedha zitakazoweza kusaidia ujenzi wa Ofisi za Kisasa.

- Kufanya mikutano kwa wanachama
   wa Vyama vya Akiba na Mikopo
   kujadili kuwa na Ofisi za Kisasa.
- Kuziunga SACCOS na Taasisi zingine za  Kifedha kwa kuzihamasisha ziwe na Mipango mikakati.

5.

Kuongeoza Idadi ya Watumishi wa Idara ya Ushirika kutoka 22 hadi Watumishi 40 ifikapo 2010.

Kuziagiza Halmashauri za Wilaya 7 saba waweze kuomba kibali Serikalini (TAMISEMI) Kuajiri Watumishi wa kada ya Ushirika.

-  Kuandikia Waraka Wakurugenzi
   Watendaji wa Halmashauri na Jiji
   juu ya haja ya kuajiri watumishi
   angalau watatu kila Halmashauri
    na Jiji.

 

 

Jedwali kuonyesha Aina mbalimbali za Ushirika katika kila wilaya mkoani.

 

S/NO

AINA YA CHAMA

GEITA

SENGEREMA

MAGU

MISUNGWI

KWIMBA

UKEREWE

ILEMELA

NYAMAGANA

JUMLA

1.

VYAMA VYA MAZAO (AMCOS)

71

74

82

40

58

14

4

3

346

2.

SACCOS

189

109

64

80

44

57

21

28

592

3.

WALAJI

NIL

NIL

NIL

NIL

NIL

NIL

1

8

9

4.

VIWANDA

3

NIL

1

4

NIL

NIL

NIL

2

10

5.

HUDUMA

NIL

NIL

NIL

1

NIL

NIL

-

13

14

6.

UMWAGILIAJI

3

NIL

NIL

4

NIL

NIL

NIL

NIL

7

7.

UVUVI

NIL

6

1

4

1

NIL

1

7

26

8.

VINGINEVYO

6

4

1

2

1

NIL

2

8

24

9.

VYAMA VIKUU

NIL

NIL

NIL

NIL

NIL

NIL

NIL

1(NCU)

* 1

10.

JUMLA

272

193

149

135

103

72

42

70

1029

Vinginevyo:
Maana yake ni vyama vya:-  Mfano: Multipurpose Coops, Madini, nyumba, Uselemala n.k)

 

 

Jedwali kuonyesha Mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi na ajira kiwilaya
mkoa wa Mwanza  - 31 July, 2007

 

S/NO

HALMA-SHAURI

MAOMBI KUZOKA KWA WANANCHI

IDADI
YA MAOMBI

KIASI KILICHO-OMBWA

KIASI KILICHO-KOPESWHA HADI 31 JULY, 2007

AINA YA BENKI

INDIVIDUAL

 SACCOS

CRDB TSHS

NMB TSHS.

1.

GEITA

NMB 968

55

1023

1,364,764,000

-

99,829,500

-

99.829,500

 

 

CRDB NIL

2

157

178,550,000

178,550,000

NIL

178,550,000

NIL

2.

 SENGEREMA

NMB 69

6

75

379,854,500

-

57,800,000

-

57,800.00

 

 

CRDB NIL

1

106

189,105,000

189,105,000

-

189,105,000

-

3.

MAGU

NMB 641

1

642

1,520,000,000

-

58,516,667

-

58,516,667

 

 

CRDB NIL

1

87

212,518,000

212,518,000

NIL

212,515,000

-

4.

MISUNGWI

NMB 40

-

40

39,000,000

-

16,900,000

-

16,900,000

 

 

CRDB NIL

-

-

-

-

-

-

-

5.

KWIMBA/
NGUDU

NMB 502

1

503

874,078,300

-

19,950,000

-

19,950,000

 

 

CRDB NIL

-

-

-

-

-

-

-

6.

UKEREWE/ NANSIO

NMB 476

9

485

531,460,000

-

12,150,000

-

12,150,000

 

 

CRDB NIL

-

-

-

-

-

-

-

7.

ILEMELA

NMB 218

-

218

655,862,300

-

140,350,000

-

140,350,000

 

 

CRDB NIL

-

-

-

-

-

-

-

8.

 YAMAGANA

NMB 2662

-

2662

8,466,228,099

-

778,900,000

-

778,900,000

 

 

CRDB NIL

1

44

63,867,000

63,867,000

-

63,862,000

-

 

JUMLA

5576

77

5998

13,831,247,199

644,037,000

1,184,396,167

644,037,000

1,184,396,167

 

Jedwali kuonyesha Hali ya vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo SACCOS
Kiwilaya mkoa wa Mwanza 31 agosti, 2007

NO

HALMASHA-URI YA WILAYA

IDADI YA   SACCOS

IDADI YA WANACHAMA

MTAJI (TSHS)

MIKOPO (TSHS)

ME

KE

JML

HISA

AKIBA

AMANA

ILIYOTOLEWA

ILIYOREJE-
SHWA

ILIYOBAKI

1.

GEITA

189

8780

58

14634

    380,429,222

22,598,900

195,968,652

1,203,777,860

698,956,245

504,821,615

2.

SENGEREMA

109

3748

2135

5883

28,703,000

69,911,000

7,375,095

427,323,940

205,080,802

222,243,138

3.

MAGU

64

 5596

8733

14329

50,897,322

297,697,985

97,029,929

1,973,601,483

576,181,633

1,397,419,850

4.

MISUNGWI

80

3073

2500

5573

145,007,000

350,970,900

85,500,000

345,000,000

304,000,000

41,000,000

5.

KWIMBA

44

3123

1990

5113

79,670,029

127,932,823.50

10,194,790

470,827,956

376,662,320

94,165,636

6.

UKEREWE

57

3604

1901

5505

72,601,000

254,328,000

11,452,000

173,442,000

105,500,000

67,947,000

7.

ILEMELA

21

2104

2120

4224

238,174,000

329,974,735

12,176,140

3,252,864,680

2,330,084,096

922,830,584

8.

NYAMAGANA

28

3500

4255

7755

148,415,000

560,885,400

9,882,120

2,158,183,997

1,084,600,660

1,073,583,337

 

JUMLA

592

33528

29488

63016

1,143,896,573

2,014,299,743.50

429,578,726

10,005,021,916

5,68 1,515,756

4,324,011,160

 
[ Ushirika ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
© 2009 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa S.L.P 119 Mwanza, Simu:028-2501037/2500366,Fax: 0282501057;Email:info@mwanza.go.tz