Mkoa wa Mwanza una Halmashauri za Wilaya tatu sita(6) ambazo ni Geita,Sengerema,Magu,Misungwi,Kwimba,na Ukerewe na Halmashauri ya Jiji la Mwanza inayohudumia wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Halmashauri za Wilaya zinaogozwa`na wenyeviti wa halmashauri na ya Jiji zinaongozwa na Mstahiki Meya, kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri husika.
Halmashauri za Wilaya za mkoa wa Mwanza pamoja na Halmashauri ya Jiji hutoa huduma za Kiuchumi zikiwepo kilimo, mifugo, misitu, Uvuvi, miuondombinu, huduma za jamii kama afya, maji, elimu, maeneo ya burudani, mazishi, mipango miji, kutunza mazingira, ustawi wa jamii, ushirika na mambo mengine yanayoihusu jamii na Taifa kwa ujumla Utawala bora ni swala linalotekelezwa na halmashauri zote katika nyanja za:
- Demokrasia
- Ushirikishwaji
- Utawala wa sheria
- Uadilifu wa viongozi na wafanyakazi wa Serikali za mitaa
- Uwazi na Uwajibikaji
- Ufanisi katika utendaji kazi
- Mchakato wa kijinsia
- Upangaji mipango
- Ujuzi wa upangaji Mipango kwa kutumia Rasilimali zilizopo
- Utekelezaji wa mipango.
|