JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
 
     
Miradi ya Maendeleo Mkoa
 
[ Miradi] [ Nyumbani ] au
 

Shabaha na malengo ya mpango wa bajeti ya maendeleo ni kama ifuatayo

  1. Kuendeleza juhudi za serikali katika kuimarisha ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ofisi za wakuu wa wilaya na Halmashauri kwa kuziogezea uwezo wa kutenda kazi, kutathimini na kufuatilia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali
  2. Kuiendeleza utekelezaji wa mikakati ya ushirikiano kati ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Taasisi na Idara zinazojitegemea katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Taasisi na Idara na ile inayotekelezwa na Halmashauri
  3. Kuziwezesha serikali za mitaa kuweka mikakati na taratibu za kuwashirikisha wananchi katika kutambua matatizo yao, kupanga na kutekeleza mipango yao ya maendeleo kupitia mfumo wa kupanga mipango shirikish na kutambua fursa na vikwazo katika maendeleo (opportunities and obstacles to development)
  4. Kuendeleza juhudi za serikali Kuu na Serikali za mitaa katika kuboresha huduma za uchumi na jamii kama ilivyoelezwa katika mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA).
  5. Kuzishauri Halmashauri kuhusu utungaji wa sheria ndogo (By laws) sheria hizo zisaidie kuimarisha usimamizi wa shughuli za maendeleo katika Halmashauri kuzishauri na kuzisaidia kuongeza uwezo na ufanisi katika kukusanya mapato, kupanga bajeti zao kulingana na mazingira ya halmashauri husika kwa kuwaendeleza wananchi katika maeneo yao na kuwapunguzia kero mbalimbali.

Miradi itakayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2008/2009

    1. Kukarabati ofisi na nyumba ya Mkuu wa Mkoa pamoja na nyumba ya Katibu Tawala wa Mkoa.
    2. Kuendeleza miradi ya kujitegemea
    3. Programu ya kuimarisha Hospitali ya Mkoa
    4. Kuimarisha mpango shirikishi na ukusanyaji takwimu
    5. Ruzuku kwa miradi ya maendeleo ya Halmashauri za Wilaya na Jiji.
    6. Kuimarisha Mpango DADP kwa kufuatilia na kushauri utekelezaji wake.
    7. Kuimarisha na kuendeleza Sekta ya Elimu.
    8. Kutekeleza Mradi wa maji safi na taka vijjini.

Ili kutekeleza miradi hiyo, mkoa unakadiria kutumia jumla ya Tshs 28,538,228,000 kati ya fedha hizi Tshs. 4,545,936,000 ni fedha za hapa nchini na Tshs. 23,992,292,000 ni fedha za nje za wafadhili.

Kwa miradi inayosimamiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa unakadiria kutumia Tshs 1,548,464,000 na kati ya fedha hizo Tshs 1,518,464,000 ni fedha za hapa nchini na Tshs 30,000,000 ni fedha itakayotolewa na wafadhili

Miradi itakayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza unakadiriwa kutumia Tshs. 4,526,929,000 na kati ya fedha hizo Tshs 170,647,000 ni fedha za hapa hapa nchini na Tshs  4,356,282,000..ni fedha itakayotolewa na wafadhili.

Miradi itakayotekelezwa na Halmashauri za Wilaya za Ukerewe, Magu, Kwimba, Missungwi Sengerema na Geita, zinakadiriwa kutumia Tshs 22,462,835,000 na kati ya fedha hizo Tshs 2,856,825,000  ni fedha za hapa nchini na Tshs 19,606,010,000 ni fedha itakayotolewa na wafadhili mbalimbali.


MUHTASARI  YA MIRADI YA MAENDELEO YA RS NA LGAs

Ufuatao ni muhtasari wa miradi ya maendeleo ofisi ya RAS                            Mradi                                                                 Tshs. Local
1.         6348    Ukarabati wa nyumba ya RC
2.         6340    Upanuzi  na ukarabati Regional  Block
3.         6349    Ukarabati wa nyumba ya RAS
4.         6339    Ujenzi wa nyumba ya DAS Ukerewe
5.         6337    Ujenzi wa ofisi ya DC-Nyamagana na Ilemela
6.         5404    Upanuzi na ukarabati Hospitali ya Mkoa
7.         4404    Ufuatiliaji programme ya DADPs 
8.         6532    Miradi ya kujitegemea (Self help scheme)
9.         6531    Mradi wa participatory appraisal
Jumla fedha ya ndani                                                                                       1,518,464,000

10.       5499    Mradi wa kupiga vita UKIMWI  
   Jumla fedha nje        30,000,000

Ufuatao ni muhtasari wa miradi ya Halmashauri za Wilaya zote sita mkoani Mwanza.
           
Code   Mradi/Mfadhili
1.         6277    Local Government Capital Dev. Grant
2.         4486    Agriculture Sector Dev. Grant
3.         3280    Rural water suppluy and sanitation
4.         6571    Urban Dev. And Environment Management
5.         4488    DASIP
6.         4203    LGTP
7.         4201    VTTP
8.         5421    Health Service Basket
9.         5499    HIV/AIDS
10.       5493    Global Fund
11.       5414    UNICEF Grant
            Jumla fedha ya nje      19,606,010,000
12.       6402    Ruzuku ya Serikali Kuu
            Jumla ya fedha ya ndani        2,856,825,000

Ufuatao ni muhtasari wa miradi ya Halmashauri ya Jiji Mwanza
Code   Mradi/Mfadhili  Tshs.
1.      6277    Local Govt. Capital Development Grant
2.      4486    Agriculture Sector Development Grant
3.      3280    Rural Water Supply and Sanitation
4.      6571    Urban Dev. And Environment Management
5.      4488    DASIP
6.      4203    LGTP
7.      5421    Health Service Basket
8.      5499    HIV/AIDS
9.      5414    UNICEF
            Jumla fedha za nje     4,356,282,000

6401    Ruzuku ya Serikali Kuu 170,647,000
       

 

 

 

 

 

 
 

MAELEZO YA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA MIRADI YA MAENDELEO

 MAELEZO YA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA MIRADI YA MAENDELEO  KWA MWAKA WA FEDHA 2008/2009 KATIKA SEKRETARIAT YA MKOA  NA HALMASHAURI ZA WILAYA NA JIJI Ili mkoa uweze kutekeleza miradi mbalimbali iliyojipangia mkoa unaomba kuidhinishiwa fedha za maendeleo kama ifuatavyo:-

1. Mradi Na.6340 UPANUZI WA OFISI YA MKUU WA MKOA

Mkoa umeidhinishiwa Tshs. 367,764,000 katika Kitengo cha Utawala ili kiweze kupanua Jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kulikarabati kutokana paa lake kuchakaa sana na baadhi ya ofisi za wafanyakazi.  Kama nilivyoeleza katika sehemu ya mapitio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya mwaka 2007/2008, jengo hili bado linahitaji upanuzi/ukarabati mkubwa kama vile, kuezeka paa kwa kutumia vigae, kukarabati ofisi za wafayakazi na kupaka rangi uzio wa jengo.  Kutokana na ufinyu wa bajeti shughuli ya ujenzi wa jengo haujakamilika ipasavyo.  Mradi huu si mpya umeanza kutekelezwa miaka miwili iliyopita. Kati ya fedha zinazoombwa katika mradi ni kwa ajili ya upanuzi wa jengo.

2. Mradi Na. 6339 UKARABATI WA NYUMBA YA RAS
Mkoa umeidhinishiwa Tshs. 45,000,000 kwa kukarabati nyumba ya RAS. Kama nilivyosema katika miradi mingine ya kukarabati majengo ya serikali, nyumba hii ilijengwa wakati wa ukoloni na kuta zake, paa, madirisha na milango inahitaji kukarabatiwa.  Kutokana na ufinyu wa bajeti mradi huu ulipangwa kufanyika kwa awamu.  Mradi huu vile vile si mpya ulianza mwaka juzi

3. Mradi Code No. 6348 UKARABATI WA NYUMBA YA RCMkoa umeidhinishiwa Tshs. 50,000,000 Katika Kitengo cha Utawala ili kiweze kukarabati nyumba ya Mkuu wa Mkoa ambayo paa lake limechakaa na servant quarter kuharibika sana. Katika mwaka 2008/2009 mkoa umepanga kukarabati nyumba ya RC kwa kuezeka paa jipya, kuendelea kukarabati sakafu ya jengo, kukarabati madirisha na milango, kuweka mfumo mzuri wa maji safi na taka. Kutokana na ufinyu wa bajeti ukarabati huu pia unafanyika kwa awamu.  Mradi huu ulianza kutengewa fedha mwaka wa fedha 2003/2004.

4.Mradi Na.6337 UJENZI WA OFISI ZA WAKUU WA WILAYA

Mkoa umeidhinishiwa Tshs. 340,000,000katika Kitengo cha Utawala ili kiweze kujenga Ofisi za Wakuu wa Wilaya ya Ilemela na Nyamagana ambao kwa sasa hawana ofisi na wanapanga kwenye majengo ya watu binafsi au Taasisi, majengo ambayo hayana hadhi ya kuwa ofisi za Serikali.  Katika mwaka 2007/2008 mkoa umepanga kumaliza kabisa ujenzi wa ofisi hii ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela kwa kuitengea Tshs…85,000,000 na zinazobaki Tshs. 255,000,000 zitatumika kuendeleza ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ambaye hana ofisi na anapanga katika jengo la H/Jiji.

5.  Mradi Na. 6532 MFUKO WA MKUU WA MKOA WA     UCHANGIAJI KATIKA MIRADI YA KUJITEGEMEA.

Mkoa umeidhinishiwa Tshs. 20,000,000 Katika Kitengo cha Utawala ili kumuwezesha Mkuu wa Mkoa kuchangia katika miradi ya kujitegemea inayoanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe. Kama nilivyosema mwanzo fedha za mradi huu zinamuwezesha Mkuu wa Mkoa kuchangia katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na wananchi na vikundi vilivyoanzisha na kutekeleza miradi yao.  Lengo la Mkuu wa Mkoa kutengewa fedha hizi ni kutaka kumfanya awaongezee ari na hamasa wananchi katika kujiletea maendeleo.  Katika mwaka 2008/2009 jumla ya miradi 50 inakadiriwa kuchangiwa.  Miradii hii itakuwa katika sekta ya ujenzi wa shule za sekondari, ujenzi wa madarasa ya shule za msingi, vyama vya akiba na mikopo (SACCOs), watoto yatima na vikundi vya akina mama na vijana na watoto yatima na walemavu.

6.  Mradi Na. 6531 USHIRIKISHWAJI JAMII

Mkoa unaomba kuidhinishiwa Tshs 5,000,000 Katika Kitengo cha Mipango na uratibu ili kuwezesha wataalam wafuatilie utekelezaji wa O & OD Participatory Planning huko wilayani. Lengo la mradi huu ni kufuatilia ufahamu na utekelezaji wa O & OD participatory appraisal.  Mradi huu ulianza mwaka juzi kufuatilia utekelezaji wa mipango shirikishi.

7.  Mradi Na. 4404 USIMAMIZI WA PROGRAMU YA DADPS

Katika kitengo cha Economic Development Support Services Mkoa unakiombea Tshs 5,700,000 ili kuwezesha wataalam wa Kitengo kufuatilia utekelezaji wa miradi ya District Agricultural Development Programme DADPS inayotekelezwa na Halmashauri. Katika mwaka 2008/2009 mkoa utatembelea Halmashauri zote na kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi na kutoa ushauri kwa Halmashauri juu ya utekelezaji wa mradi.  Mradi huu si mpya ulianza mwaka wa fedha wa 2006/2007.

8. Mradi Na. 6239 UPANUZI WA HOSPITALI YA MKOA

Mkoa unakiombea Kitengo cha Curative Services kiasi cha Tshs. 600,000,000 Ili kiweze kuendelea kuipanua hospitali ya mkoa ambayo ni muhimu sana kwa huduma za afya kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza. Katika mwaka 2008/2009 mkoa utaendelea na mpango wake wa upanuzi wa hospitali kwa kukarabati baadhi ya maward na sehemu ya mapokezi.  Pia utachagia katika mradi wa UKIMWI ulioanzishwa hapa hospitalini.

KIFUNGU Na. 8091 Ruzuku kwa Miradi ya Maendeleo ya Halmashauri za Wilaya na Miji Tshs. 26,989,764,000

9.  Mradi Code No. 6401
Mkoa unaziombea Halmashauri za Wilaya Tshs. 22,462,835,000  ili ziweze kutekeleza Miradi ya Maendeleo walinayojiwekea kwenye mipango yao iliyopitishwa na Mabaraza  yao ya Madiwani.  Kati ya fedha hizo Tshs 2,856,825,000. zitatolewa na serikali Kuu na Tshs 19,606,010,000 ni fedha za nje.

10. Mradi Code No. 6402 Mkoa unaiombea Halmashauri ya Jiji la Mwanza Tshs. 4,526,929,000. Ili liweze kutekeleza Miradi ya Maendeleo walinayonayo kwenye mipango yao iliyopitishwa na Madiwani wao.  Kati ya fedha hizo Tshs 170,647,000 zitatolewa na Serikali Kuu na Tshs 4,356,282,000 itatolewa na wafadhili mbalimbali.

 

11.  Mradi code 6339 Mkoa unaomb jumla ya Tshs 85,000,000 kuanza ujenzi wa nyumba ya DAS wa Wilaya ya Ukerewe katika mwaka wa fedha 2008/2009.  Nyumba ya DAS ilijengwa  kwa kutumia udongo wa tope hivyo haiwezi kukarabtika kutokana na uchakavu mmkubwa wa nyumba hiyo.

 

 

 
 
 
[ Miradi ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
© 2009 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa S.L.P 119 Mwanza, Simu:028-2501037/2500366,Fax: 0282501057;Email:info@mwanza.go.tz