 |
 |
 |
|
Idara ya Mipango ina majukumu ya Kuratibu, kufuatilia na kutoa huduma katika nyanja mbalimbali, yafuatayo ni majukumu ya Idara hii:
- Kuratibu masuala yote ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
- Kuratibu Mipango na Bajeti ikiwemo Mpango Mkakati na Mipango kazi.
- Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja.
- Sekretarieti katika vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).
- Kuunganisha, kuratibu na kufuatilia Mipango na Bajeti za Serikali za mitaa.
- Kutoa huduma za kitaalam katika utekelezaji wa Mfumo wa habari na mawasiliano.
- Kuratibu miradi ya Wahisani mkoani
- Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa juu ya masuala ya mashirika ya Umma, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi
- Kuratibu shughuli za utafiti mkoani
- Kuratibu zoezi la Sensa.
- Kuziwezesha mamlaka za Serikali za mitaa juu ya utekelezaji wa sheria ya mazingira Na. 2 ya 2004.
- Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa na Halmashauri juu ya utekelezaji wa sheria za kazi.
- Kuratibu masuala ya Maafa katika mkoa.
|
MIPANGO YA MAENDELEO YA MKOA WA MWANZA 2009/10 |
Upanuzi wa jengo la Utawala
Upanuzi wa Hospitali ya Mkoa-SeKou Toure
Ujenzi wa Ofisi ya mkuu wa wilaya ya yamagana
Uratibu wa Mipango ya Kuboresha Kilimo-ASDP
Uratibu wa Mipango ya Kilimo -DASIP
Mfumo shirikishi wa Jamii-Participatory Appraissal
Mfuko wa mkuu wa Mkoa
Kuchangia Miradi ya Maendeleo
|
| |
|
|
MIPANGO |
|
| |
Mipango katika Tanzania inatekelezwa katika ngazi mbalimbali.
Katika ngazi ya Taifa kuna agenda za Muda mrefu (Framework) za kitaifa .Hii ni mikakati ambayo imeandaliwa kwa ajili ya maamuzi ya jumla kama dira ya Pamoja kwa siku zijazo.Mifano ya mikakati hii ya kiataifa ni VISION 2025,Mpango Mkakati wa Muda wa Kati (Medium Term Plan) na Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA ). Chini ya ngazi taifa kuna Mipango ya Kitaasisi.abla ya mkukuta kulikuwa na mipago mbalimbali hivyo MKUKUTA ni jitihada mbadala ya Tanzania katika kupunguza umasikini,mikakati ya awali ilikuwa na dhana finyu ya umaskini ambapo MKUKUTA umejikita Katika imani kuwa umasikini ni suala mtambuka na pana na suluhisho lake ni mikakati yenye mawanda mapana ,hivyo ni suluhisho limejikita katika Nyanja tatu (3) ambazo ni;
- Kukuza kipato na kupunguza maskini.
- Kuboresha Maisha na Ustawi wa jamii.
- Utawala Bora na Uwajibikaji.
MKUKUTA kama zana ya upangaji ina malego makuu mawili;
- Unafanya kazi kama muongozo wa kufikiwa kwa matokeo ya kukua kwa kipato na kupunguza Umaskini pia kama muogozo wa hatua za kuchukuliwa kama vipau mbele vya kukuza kipato na kupunguza umaskini katika serikali,asasi za kiraia na sekta binafsi.
- Unaelekeza kuelekeza fedha za umma kweye hivyo vipaumbele.
Mfumo wa Menejimenti ya Ufanisi (Performance Management System- (PMS) kupitia Dhana ya Kuboresha Ufanisi (Performance Improvement Model)-PIM,inayosimamiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma-OR-MUU inayokusudia kuboresha Ufanisi wa Wizara,Idara na wakala wa serikali (MDAs),Sekretarieti(RSs) za mikoa na Mamlaka za serikali za Mitaa (LGAs ). Kupitia utaratibu huu serikali imeamua kuwa Wizara,Idara na wakala wa serikali (MDAs),Sekretarieti(RSs) za mikoa na Mamlaka za serikali za Mitaa (LGAs ) zote kuwa na Mipango mikakati (Strategic Plans/Institutional Plans) inayo onyesha/bainisha mwelekeo wa kufikia malengo na majukumu yake katika muda wa kati,vile vile hii ina tekeleza malengo ya maendeleo ya Milenia,Dira ya Taifa ya Maendeleo(Vision 2025) na nyanja zingine muhimu. Mipango hii inabainisha ni matokeo gani Taasisi inatarajia kufanya,nini ifanye na kwa sababu zipi,Mpango mkakati ni mpana zaidi ya MKUKUTA.
Mpango mkakati (Strategic Plan-SP) wa taasisi yeyote una sifa kuu zifuatazo:
- Uchambuzi wa hali halisi ilivyo (Situational analysis) hii huuangalia asili ya taasisis,majukumu na kazi za taasisi ,Uchambuzi wa Wadau na Tathmini ya ndani na nje ya Taasisi kwa kutumia utaratibu wa “SWOC/SAOC”
- Dira ya Taasisi.
- Mwelekeo
- Malengo
- Mikakati (Strategies)
- Shabaha (Targets)
- Vigezo vya kupima Ufanisi (Performance Indicators)
Mpango huu wa mipango unawapa nguvu wananchi katika kufanya maamuzi katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.Katika ngazi za serikali za mitaa mchakato wa mipango unafuata methodolojia ya muongozo wa Fursa na vikwazo vya maendeleo “Opportunities and Obstacles to Development-(O&OD)”.Ni mpango shirikishi jamii wa Upangaji mipango wenye sifa zifuatazo;
- Ni methodolojia inayoanzia chini kuja juu(bottom up methodology)
- Inaanza na Fursa badala ya vikwazo ili kukuza ari kuanza na fursa zilizopo katika eneo husika na kuamusha kujitegemea na kumiliki maedeleo kwa jamii yenyewe.
- Inajenga daraja kati ya Serikali za mitaa/Vijiji na Halmashauri zenyewe( LGAs).
- Inafanya kazi ndani ya muundo wa Halmashauri( LGAs)na kuzingatia Mipango ya jumla ya kitaifa.
- Inawawezesha kuandaa mipango yao kwa kutumia dira ya maedeleo ya Taifa ya 2025.
- Ina shirikisha sekta nyingi (multi-sectoral)
- Inajega uwazi na uwajibikaji (Transparency and accountability)
- Inazi wajibisha Serikali kuu na za mitaa kukidhi/kutatua mahitaji wa jamiiIt helps
- Serikali za mitaa zinaratibu shughuli za wadau wa maendeleo.
- Ina jenga uwezo wa jamii kutatua masuala ya mtambuka.( cross- cutting issues)
- Inakuza mahusianao kati ya sekretarieti ya mkoa a serikali za mitaa kupitia kujenga uwezo.
|
| |
|
VIPAU MBELE VYA MKOA WA MWANZA |
Na. |
Jina la mradi |
Gharama (Tshs) |
1. |
Upanuzi wa Jengo la Regional Block |
1,500,000,000 |
2. |
Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nyamagana |
800,000,000 |
3. |
Ununuzi wa Boat 2 Ukerewe na Sengerema |
600,000,000 |
4. |
Ujenzi wa ofisi za Makatibu Tarafa Tshs.40,000,000 |
5,320,000,000 |
|
Halmashauri ya JIJI LA MWANZA
Na. |
Jina la mradi |
Gharama (Tshs) |
1. |
Ujenzi wa vyumba 180 vya madarasa ya shule za sekondari |
1,500,000,000 |
2. |
Uendelezaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Butimba |
750,000,000 |
3. |
Upanuzi wa mto mirongo (kujenga kuta km.6) |
6,500,000,000 |
4. |
Ujenzi wa barabara ya kijiji – Kiloleli (km.3) kwa kiwango cha lami |
2,500,000,000 |
5. |
Ujenzi wa barabara inayoelekea Chuo cha Ualimu cha Butimba (km. 2.5) kwa kiwango cha lami |
2,000,000,000 |
6. |
Ujenzi (Upgrading) wa Barabara zinazoelekea shule mpya za sekondari |
500,000,000 |
7. |
Ujenzi wa Agricultural Resource Centre ya Sangabuye |
30,000,000 |
|
Uanzishaji wa Benki ya wananchi ya Mwanza (Mwanza Communicy Bank) |
250,000,000 |
8. |
Uanzishaji wa ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Ilemela |
1,000,000,000 |
9. |
Ujenzi wa josho la fumagila |
35,000,000 |
10. |
Ulipaji wa fidia ya Ardhi na mimea |
800,000,000 |
11. |
Ujenzi wa miradi ya Maji ya Igombe, Kayenze na Buhongwa |
1,500,000,000 |
12. |
Ununuzi wa skip loaders 2 kwa ajili ya kubeba taka ngumu |
380,000,000 |
|
Jumla |
17,745,000,000 |
|
HALMASHAURI YA WILAYA YA KWIMBA
Na. |
Jina la mradi |
Gharama (Tshs) |
1. |
Uejnzi wa vyumba 28 vya madarasa |
340,2000,000 |
2. |
Ukamilishaji wa nyumba za walimu 15 |
288,000,000 |
3. |
Ujenzi wa maabara 1 |
36,000,000 |
4. |
Ukarabati wa vituo 2 vya Afya |
104,000,000 |
5. |
Ukarabari wa Zahanati 12 |
224,000,000 |
6. |
Ujenzi wa Zahanati 5 |
105,000,000 |
7. |
Ujenzi wa visima virefu vya maji |
25,000,000 |
|
Ujenzi wa matanki ya kuvunia maji ya mvua (Sekondari) |
54,000,000 |
8. |
Uimarishaji wa mradi wa Maji Mjini (Ngudu) |
50,000,000 |
9. |
Ujenzi wa nyumba 4 za watumishi |
220,000,000 |
10. |
Ukarabati wa jengo (Boma) la Halmashauri |
28,000,000 |
11. |
Uimarishaji wa km za barabara |
233,428,000 |
12. |
Ujenzi wa madaraja |
80,500,000 |
|
Jumla |
1,788,528,000 |
|
| |
HALMASHAURI YA WILAYA YA UKEREWE
Na. |
Jina la mradi |
Gharama (Tshs) |
1. |
Kukarabati jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya awamu ya pili |
320,000,000 |
2. |
Kujenga nyumba 5 za watumishi |
190,000,000 |
3. |
Kujenga vyumba vya madarasa katika shule za msingi 60 |
186,000,000 |
4. |
Kujenga nyumba za walimu 10 shule za msingi |
45,000,000 |
5. |
HIV/AIDS |
145,000,000 |
6. |
Kununua boti 1 iendayo kwa kasi |
130,000,000 |
7. |
Kununua gari la taka ngumu |
110,000,000 |
8. |
Kununua gari (lori) kwa ajili ya Idara ya Elimu |
110,000,000 |
9. |
Kuendesha mpango wa O & OD |
45,000,000 |
10. |
Uendelezaji kilimo (District Agriculture Development Support) |
135,000,000 |
11. |
Kujenga bwawa la maji machafu (sewerage lagoon) |
150,000,000 |
12. |
Uimarishaji wa km za barabaraUkarabati wa zahanati/vituo vya afya |
57,000,000 |
|
Jumla |
1,623,000,000 |
|
| |
HALMASHAURI YA WILAYA MISUNGWI
Na. |
Jina la mradi |
Gharama (Tshs) |
1. |
Mradi wa maji toka ziwa Victoria |
2,000,000,000 |
2. |
Kujenga nyumba za watumishi 10 (wakuu wa idara) |
500,000,000 |
3. |
Ujenzi wa ukumbi wa Halmashauri |
100,000,000 |
4. |
Ununuzi wa gari kwa ajili ya uratibu wa miradi |
100,000,000 |
5. |
Gharama za upimaji viwanja |
50,000,000 |
6. |
Mkopo kwa ajili ya fidia ya viwanja |
185,000,000 |
7. |
Ujenzi wa hospitali ya Wilaya |
1,500,000,000 |
8. |
Ununuzi wa ambulance na gari moja (kila moja 100,000,000) |
200,000,000 |
9. |
Kujenga madarasa 82 ya sekondari za kata |
574,000,000 |
10. |
Kujenga maabara 20 |
540,000,000 |
11. |
Kujenga nyumba za walimu 60 |
840,000,000 |
|
Jumla |
6,589,000,000 |
|
| |
HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA
Na. |
Jina la mradi |
Gharama (Tshs) |
1. |
Ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa ya ‘A’ level |
8,750,0000 |
2. |
Ujenzi wa maabara 3 za shule za sekondari |
60,884,344 |
3. |
Ujenzi wa vyumba 30 vya madarasa ya sekondari |
382,352,335 |
4. |
Ukamilishaji wa nyumba za walimu wa sekondari |
339,001,254 |
5. |
Ukamilishaji wa madarasa 6 ya shule za msingi |
25,530,000 |
6. |
Ukamilishaji wa vyumba 2 vya madarasa /Msingi |
8,400,000 |
7. |
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya |
78,750,000 |
8. |
Ukamilishaji OPD Luchili na Karumo |
14,700,000 |
9. |
Ukamilishaji nyumba za watumishi |
32,655,000 |
10. |
Ukarabati wa zahanati na vituo vya Afya |
685,461,063 |
11. |
Matengenezo ya kawaida |
183,810,000 |
12. |
Matengenezo ya sehemu korofi |
123,604,800 |
13. |
Matengenezo ya muda maalum |
226,000,000 |
14. |
Madaraja na makalvati |
63,975,2000 |
15. |
Uendelezaji kilimo cha pamba |
12,159,910 |
16. |
Uzuiaji magonjwa na visumbufu vya mimea |
4,800,000 |
17. |
Uendelezaji ushirika |
6,000,000 |
18. |
Uendelezaji Kilimo cha Wafanyakazi |
12,099,395 |
19. |
Uzuiaji magonjwa ya wanyama |
15,356,173 |
20. |
Kupambana na kichaa cha mbwa |
4,800,045 |
21. |
Ununuzi wa gari kwa shughuli za ugani |
70,779,072 |
22. |
Uendelezaji kilimo cha umwagiliaji |
42,918,249 |
23. |
Uendelezaji mazao mchanganyiko ya Biashara |
32,091,925 |
24. |
Uimarishaji wa miundombinu ya mifugo |
44,400,000 |
25. |
Miundombinu ya DASIP |
293,155,000 |
26. |
Ukarabati wa miundombinu ya Maji |
631,000,000 |
27. |
Ukarabati wa Ofisi ya Maji |
52,000,000 |
|
Jumla |
3,505,433,765 |
|
| |
|