JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
 
     
SEKTA YA MAJI :
 
[ Maji ] [ Nyumbani ] au
 

Hali ya upatikanaji maji kwa matumizi ya binadamu mkoani Mwanza siyo nzuri, ikichangiwa na uharibifu mkubwa wa mazingira. Hata hivyo, pamoja na hali hiyo, vyanzo vya kuaminika vya maji katika mkoa huu vinajumuisha: Ziwa Victoria, rasilimali ya maji ardhini (Visima virefu, vya kati, vifupi na vya asili), Mito, Mabwawa ya maji ya kujengwa, chemichemi na uvunaji wa maji ya mvua kwa paa za nyumba.
    Miradi ya aina mbalimbali ya maji safi na salama inaendelezwa katika wilaya zetu. Chanzo cha maji cha Ziwa Victoria ambacho ni cha kuaminika bado hakijatumika ipasavyo hata katika kumpatia maji mwananchi anayeishi kando kando ya ziwa hili. Hali ya usafi wa maji katika ziwa hili siyo nzuri na, kwa kweli chanzo hiki bado hakijanufaisha ipasavyo wakazi wa mkoa huu katika kuwapatia maji safi na salama. Katika mkoa, kuna miradi ya maji ya bomba ipatayo 40 kutoka kwenye chanzo cha Ziwa Victoria na mingi ya miradi hiyo haifanyi kazi kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo ukosefu wa mitambo na pengine na uhaba wa madawa ya kusafishia maji hayo na hususan ukosefu wa fedha.

kabla ya mvua za msimu huu tulikuwa na tatizo la kupungua kwa kina cha maji katika ziwa Victoria kutokana na ukame (mvua kutokunyesha ipasavyo miaka ya nyuma) na pia kujaa kwa tope ziwani. Upungufu huu wa kina ulisababisha kupungua kwa huduma ya maji jijini baada ya bomba la mtiririko Capri Point kutokeza nje juu ya maji. Pia chanzo cha maji cha Mji wa Sengerema, mradi wa Nyamazugo, chanzo cha maji cha mji wa Magu kwenye eneo la Busulwa n.k. viliathirika na kushuka kwa kina cha ziwa Victoria. Hivi sasa kina hiki kimeongezeka kwa karibu cm 120 kiasi ambacho kimerejesha huduma za maji katika hali ya kuridhisha.
       Tatizo la gugumaji limeanza kujitokeza tena katika ziwa Victoria, na hivi karibuni ilivamia tena pwani ya ziwa maeneo ya hapa jijini kiasi cha kuathiri shughuli za wavuvi wadogo wadogo na hata kituo cha

 
 

MATATIZO YA GUGUMAJI

Matatizo ya gugumaji ni pamoja na:-
  1. Kuharibu upatikanaji wa maji safi kwa matumizi ya nyumbani, Mifugo, wanyamapori, viwanda na kuharibu mazingira
  2. Kuathiri huduma za usafiri na usafirishaji wa watu na mizigo katika ziwa Victoria
  3. Kuathiri shughuli za uvuvi na mazalio ya samaki.  Aidha yanahusika sana kuharibu bioanuawai ya ziwa
  4. Pia yanahifadhi viumbe na vimelea vya magonjwa yaenezwayo kwa njia ya maji kama vile kichocho na homa ya matumbo na matatizo ya kiafya kwa binadamu.
    Kutokana na matatizo yanayosababishwa na gugumaji, Kitengo cha Udhibiti wa Gugumaji chini ya “Lake Victoria Environmental Management Programme” (LVEMP) Taasisi iliyo na ofisi zake hapa jijini. Njia zinazotumika kudhibiti gugumaji ni pamoja na:-
    1. Njia za kibaolojia kwa kutumia wadudu washambuliao gugumaji wanaoitwa mbawakavu (Neochetina Weevils)
    2. Kuopoa gugumajji kwa kutumia nyenzo rahisi za mikono kama vile reki, matoroli mapanga majembe na mitego
    3. Kuelimisha jamii kuacha kueneza gugumaji.
      Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kudhibiti gugumaji utafiti uliofanyika Novemba na Desemba, 2006 ulionyesha kwamba asilimia 75 ya gugumaji ilikuwa imeongezeka tena kwenye ziwa kutoka kiasi cha Hekta 400 zilizoripotiwa mwaka 2004 hadi kufikia Hekta 700 mwaka 2006. Gugumaji linaingizwa kwa wingi katika ziwa kutoka mto Kagera na mto Mara ambapo inakadiriwa kuwa Hekta mbili (2) huingizwa ziwani na mito hiyo.  Sababu nyingine kubwa ni kwamba yapo maeneo kumi na saba (17) ambapo gugumaji limekuwa sugu na kufanya mbawakavu wanaopandikizwa kushindwa kudhibiti magugumaji hayo.

UDHIBITI WA MAGUGUMAJI

Harakati za vyombo vinavyohusika na kudhibiti gugumaji vinafanya hivyo kupitia mikakati ifuatayo:-
1.Kudhibiti kuenea kwa gugumaji kutoka katika vyanzo vya mto Kagera na mto Mara
2.Kuendelea na utafiti kupata sababu ambazo zinafanya mbawa kavu wasistawi katika mito ya Kagera na  Mara.
3.Kuwa na programmu ya ufuatiliaji na udhibiti wa gugumaji (Regional/ National Surveillance Programme)  kwa kuzishirikisha nchi za Rwanda na Burundi.
4.Kuendelea kuzalisha na kupandikiza mbawakavu
5.Kuendelea kuelimisha jamii kutosambaza gugumaji

 

Jedwali likionyesha Vyanzo vya Maji katika Mkoa wa Mwanza

Vyanzo/
Miradi
Ya maji

Wilaya

Jumla

Vinavyofanya kazi

Vilivyokauka/Kuto-fanya kazi

Bila ya Pampu

Magu

Kwimba

Misungwi

Sengerema

Geita

Ukerewe

Jiji

Visima Vifupi na vya kati

844

678

308

206

301

136

168

2,641

2,409

184

48

Visima Virefu

23

57

33

5

85

-

41

244

207

33

2

Mabwawa ya Maji

1

1

1

2

2

-

-

7

2

5

-

Ziwa Victoria

8

-

5

7

4

8

6

38

20

18

-

Visima vya Asili (Improved Tradtional Water Sources)

44

32

27

45

-

19

86

274

248

26

-

 
 
[ Maji ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
© 2009 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa S.L.P 119 Mwanza, Simu:028-2501037/2500366,Fax: 0282501057;Email:info@mwanza.go.tz