JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
 
     
Bajeti
 
[ Maji ] [ Nyumbani ] au
 

Kimsing , bajaeti ni mchakato wa kugawa raslimali kwa namna nzuri zaidi ya mpago.Kwa maneno mengine bajeti ni namna ya kuufanya mpango ufanye kazi i.e. Ni mchakato wa kubadilisha mipango kuwa katika mfumo wa fedha.Ni kazi endelevu inayojibu swali nii kifanyike ili kukamilisha mpango kazi kwa ufanisi zaidi.
    Mpango wa matumizi wa muda wa Kati (MTEF) uliaza kama jitihada za bajeti ya oparasheni maalumu lakini kadiri siku zinavyokwenda imekuwa ikitumika kama zana ya kufanyia mipango(planning tool). MTEF ulibuniwa kwa ajili ya kuleta ufanisi kwenye kugawa raslimali na uko chini ya wizara ya Fedha na Uchumi.Ni lazima kwa Wizara,Idara,Wakala(MDAs) na Mamlaka za serikali za mitaa(LGAs)It is an obligation that MDAs, RSs and LGAs kuandaa bajeti zake kwa kufuata utaratibu wa MTEFU ambao kimsingi umegawanyika katika sehemu kuu nne(4) ambazo ni :

  1. Malengo (Objectives)
  2. Shabaha (Targets)
  3. Activities and
  4. Vitendea kazi (Inputs).
MTEF umekuwa ni injini/muhimili wa mchakato wa upangaji mipango serikalini. Kupitia utaratibu huu raslimali zinagawanywa na mipango inatekelezwa.
       MTEF ni vipaumbele vya miaka mitatu vya makisio kwa pamoja (matumizi ya kawaida a maendeleo,vyanzo vya serikali na wadau wa maendeleo) ambao umejikita kwenye viashiria vya ufanisi katika mpango mkakati(strategic plan).Ni mchanganyiko wa mpango unaotekelezwa(rolling plan) na bajeti ijayo (forward budget (RPFB)) na Bajeti ya ufanisi(performance budget).
      Malengo mahususi ya MTEF ni:
  1. Kuifanya bajeti itabirike kwa kuchochea ukusanyaji wa vyanzo vya mapato vya ndani ,kuweka pamoja fedha za nje kuhakikisha uwiano ili kuendana na mgawanyo unaokubalika unaozingatia vipaumbele.
  2. Kuwezesha kujitoshereza kibajeti kwa kuhakikisha kuwa gharama za utekelezaji wa shughuli zina zinabebeka kwa kutumia raslimali zilizopo na za baadaye.
  3. Kupunguza utegemezi wa bajeti kutoka kwa wahisani wa Miradi/Programu kuwezesha ugawaji wa raslimali kwenye uwekezaji na matumizi megine.
  4. Kuimarisha bajeti yenye kuzingatiamatokeo(output oriented budget) ambayo inalenga katika kuboreshautoaji wa huduma bora.
Uwasilishaji wa Mipango na Bajeti:
  1. Mipango na bajeti za Vijiji/kata katika Timu ya Menejimenti ya Halmashauri( Council Management Team) kwa ajili ya uchambuzi, vipaumbele na kuwekwa pamoja( consolidation).
  2. Mkurugenzi wa Halmashauri (Council Director) kuwasilisha mipango na bajeti kwenye Timu ya Menejimenti ya Mkoa (Regional Management Forum) kwa ajili ya ushauri wa kiataalamu.
  3. Mipango na Bajeti kuwasilishwa kwenye Kamati ya Ushauri ya Wilaya(District Consultative Committee)
  4. Mipango na Bajeti kuwasilishwa kwenye Kamati ya Ushauri ya Mkoa(Regional Consultative Committee)
  5. Mipango inarudishwa kwenye kamati ya Fedha ya Halmashauri husika.
  6. Mipangoa na Bajeti kuwasilishwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani( Full Councils) husika kwa ajiri ya kupitishwa
  7. Mipango na Bajeti kuwasilishwa kwenye Sekretariati ya mkoa husika kwa majumuisho (consolidation).
  8. Mipango na Bajeti kuwasilishwa Wizara ya Fedha (MOFEA) na Wizara ya TAMISEMI(PMORALG) kwa uchambuzi.
  9. Wizara ya Fedaha na Uchumi(MOFEA) huwasilisha Mipango na Bajeti kwenye Kamati ya kitaalamu ya wizara (Inter Ministerial Technical Committee) na Baraza la Mawaziri kwa uthibitisho.
  10. TAMISEMI na RS kuwasilisha Mipango na Bajeti Kwenye Kamati ya Bunge ya Kisekta .
  11. Mipango na Bajeti huwasilishwa Bungeni kwa uthibitisho wa mwisho.

 

 
 

Raslimali Fedha

                   
Mhasibu wa Mkoa ( Regional Accountant) ana wajibika moja kwa moja kuongoza kitego cha fedha na Uhasibu ambacho kazi yake kuu ni kutoa huduma bora za menejimenti ya fedha na utunzaji vitabu vya fedha (quality financial management and bookkeeping services) kwenye Sekretarieti ya mkoa (RS)

MAJUKUMU MAKUU (MAIN ACTIVITIES )

  • Kusimamia utendaji wa idara ya fedha na uhasibu ( Finance and Accounting Unit) ya sekretarieti ya Mkoa (RS)kwa lengo la kuwa na mfumo wa fedha wenye Tija.
  • Kukuza ufanisi wa kitengo cha Mipango na Fedha kwa kuhakikisha kuwa utendaji kazi wa kitego uaedana na Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali .
  • Kusimamia michakato ya ukusayaji wa Fedha na kuzipeleka Benki kwa mujibu wa Kanuni za Fedha na Taratibu za uhasibu za serikali.
  • Kthibitisha malipo yote yanayoplipwa na Sekretariti ya mkoa (RS) na kuhakikisha yanafanyikwa kwa mujibu wa Bajeti iliyopitishwa ,Kanuni za serikali na Taratibu za Kiuhasibu
  • Kitamshauri Katibu Tawala wa mkoa(RAS) mara kwa mara juu namna bora ya kutekeleza na kuendana na kanuni za fedha,Tartibu za kihasibu na Kimanunuzi za serikali (government financial regulations and accounting and procurement procedures) mara ithibitikapo kukiukwa.
  • Kitatekeleza majukumu yeyote kwa mujibu wa Kanuni za Fedha Sehemu ya kwanza na ya Pili (Financial Orders Part I & III) au kama itakavyoelekezwa na Katibu Tawala wa Mkoa( RAS).

Aidha kitengo pia kitafanya majukumu yafuatayo:

  1. Kupokea na Kuweka Benki mapato yote ya serikali.
  2. Kuandaa Mizania ya Fedha.
  3. Kuandaa Taarifa za Fedha za Mwezi,Robo Mwaka ,Nusumwaka na za Mwaka ( monthly, quarterly, half yearly and annual financial reports).
  4. Kuandaa majibu ya Hoja za Kamati ya Hesabu za Serikali( Public Accounts Committee) juu ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG t;kuratibu majibu ya hoja zote za Ukaguzi.
  5. Kuzichunguza Vocha zote za Malipo.
  6. Kufanya Malipo yote ya Bajeti ya Sekretarieti ya Mkoa .
  7. Kufuta rekodi vifungu (accounts) kwa mujibu wa Mwongozo wa Fedha ( Financial Order Part I (1.1.1)).
 
 
    Mzunguko wa Upangaji na Uandaaji Bajeti

KAZI (ACTIVITY)

Muda Katika Majuma
(DURATION IN WEEKS
)

Miezi (TIMING)

  1. Kuandaa na Kutoa Mwongozo wa Taifa waBajeti.
  2. Kutathmini Mchanganuo wa Fursa na Vikwazo vya Maedeleo (O & OD ) kama mchango kwenye Mipango ya Maedeleo ya Halmashauri.
  3. Mikoa kuzijulisha halmashauri husika juu ya mahitaji ya kitaalamu kwa ajili ya Mchakato wa Bajeti.

 

Novemba-Desemba

  1. Serikali za Mitaa Pamoja na Sekretarieti za mikoa kuandaa Mipango na Bajeti zao.

 

Januari-Februari

  1. Mamlaka za Serikali za mitaa(LGAs) na Sekretarieti za mikoa kuwasilisha Mipango na Bajeti zao kwenye Kikao cha Menejimenti ya Mkoa (RMF) na Wizara ya Fedha na Uchumi kwa ajiri ya uchambuzi.
  2. Mamlaka za serikali za Mitaa (LGAs) kuwasilisha Mipango na Bajeti zilizochambuliwa kwenye kamati za ushauri za wilaya (DCC) na Mkoa (RCC) kwa Maboresho zaidi.
  3. Mamlaka za serikali za Mitaa (LGAs) kuwasilisha mipango na Bajeti kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ( Full Council) kwa Uamuzi wa Mwisho ( approval)

 

Machi- Aprili 

  1. Kuwasilisha Majumuisho ya Mipango na Bajeti za mikoa kwenye Kamati ya Kikatiba ya Bunge.

 

Mei

  1. Bunge kupitisha Mipango na Bajeti kwa Mwaka husika wa fedha .
  2. Kuandaa Mpango kazi.

 

Juni

  1. Kuwasilisha taarifa za majumuisho ya Robo Mwaka ya mikoa Wizara ya fedha na Uchumi na TMISEMI.

 

Octoba, Januari, April and Julai

 

 
 
 
[ Fedha_Bajeti ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
© 2009 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa S.L.P 119 Mwanza, Simu:028-2501037/2500366,Fax: 0282501057;Email:info@mwanza.go.tz