Mbio za Mwenge wa uhuru zimezunduliwa kitaifa Mkoani Mbeya tarehe 11 Mei 2012. Mwenge huo unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya zote 133 Tanzania, kauli mbiu ya mwaka huu ni “sensa na makazi ya watu, maboresho ya katiba, kupambana na rushwa, ukimwi na dawa za kulevya”. Kwa Mujibu wa Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Mwanza Ndugu. Diana Rwechungura Mwengea wa uhuru unatarajiwa kuwa mkoani Mwanza kuanzia tarehe 19-26 Agosti 2012 na utazindua Miradi mbalimbali ya Maendeleo. |