JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
 
 
 
 .: Umbile la Utawala
 .: Historia ya Mkoa
 .: Dira&Mwelekeo
 .: Miradi & Programu
 .: Fedha & Bajeti
 .: Nyaraka Mbalimbali
 .: Mipango
 .: Takwimu
 .: Kilimo na Mifugo
 .: Maliasili&Mazingira
 .: Elimu
 .: Afya
 .: Maji
 .: Ushirika
 .: Biashara
 .: Barabara na Majengo
 .: Ardhi
 .: Jamii, Jinsia & Watoto
 .: Taarifa za Mkaguzi
 .: Kazi
 .: Sheria
 .: Serikali za Mitaa
 .: FAQs & Mijadala
.: Kamati ya Uhariri
.: Watumishi wa Mkoa
.: TEHAMA (ICT)
.: Tovuti Zingine
 

Dr. Faisal Issa
Katibu Tawala(M) Mwanza
 
     

RC Akiwa Ofisini Kwake

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh. Zainab Telack Akihutubia Wananchi Katika kilele cha wiki ya Maji .

Mheshiwa Zainab Rajab Telack width=

WATAALAM WAMETAKIWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI VIZURI.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amewataka wahandisi wa miradi ya Maji katika Halmashauri na miji midogo mkoani hapa kusimamia vizuri miradi ya maji na kwamba fedha zitakazotumika kwenye miradi hiyo zitumike vizuri ilikusaidia ikamilike katika viwango vinavyotakiwa.


Akizungumza kwa kwenye kilele cha maji mkoani hapa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Zaibabu Terack kwenye sherehe za kilele cha maji zilizofanyika Wilaya ya Sengerema, Mulongo alisema kuwa miradi ya maji Mwanza inaweza kukamilika kwa wakati kama fedha za miradi hiyo zitatumika vizuri.


Alisema kazi ya kusimamia miradi hiyo inapaswa kufanywa na wakandarasi wa Halmashauri na miji midogo ambayo inapitiwa na miradi hiyo na kwamba kama fedha za miradi zitatumika kinyume Mwanza itaendelea kuwa na tatizo la maji. “Naomba niwaombe Wakandarasi wa maji kutoka Halmashauri zote za Mwanza pamoja na miji midogo ambayo inapitiwa na miradi ya maji isimamie vizuri miradi hiyo.Nataka kuona fedha za miradi zinatumika vizuri na miradi yote inatekelezwa kwa wakati,”alisema Mulongo na kuongeza:


“Kama tutakwenda kinyume na matumizi ya fedha za miradi ya maji tutaendelea kuwa na tatizo la maji na kero za maji ambazo zinawakabili wananchi zitaendelea, hivyo sitakubali kuona wananchi wanateseka kwa kukosa maji wakati Serikali yao inawajali kwa kuwaletea miradi ya maji.” Akisoma taarifa ya miradi ya maji, Katibu tawala msaidizi maji Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Warioba Sanya, alisema Serikali imewekeza Sh.84.46 bilioni kwa ajili ya miradi ya Maji ya mkoa wa Mwanza kupitia mapango wa maji wa (WSDP).


“Mwanza tunaishukuru Serikali, kwani licha ya kutupa miradi mbalimbali ya maji Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya maji vijijini 217 kati ya hiyo miradi 140 imekamilika sawa na asilimia 65 na kwamba miradi iliyobaki itakamilika ifikapo mwezi juni mwaka huu,”alisema Sanya.


Mkoa wa mwanza kwa hivi sasa unawapatia maji wananchi kwa asilimia 61.

 

HABARI NYINGINE  
     
Nafasi za Kazi / Ajira  
  .....................................................  
Zabuni na Minada  
  .....................................................  
V V U / UKIMWI  
Bodi ya Utalii  
  .....................................................  
  .....................................................  
Fursa za Uwekezaji  
  .....................................................  
     
 
  Matukio Yajayo :  
 
       
Mei Mosi
01/05/2015
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
26/04/2015
Karume Day.
07/04/2015
Sikuu ya Pasaka.
06/04/2015
Ijumaa Kuu.
03/04/2015
Siku ya UKIMWI Duniani.
01/12/2014
............................................................................................................
  Kwa matukio yajayo zaidi Bonyeza hapa kusoma zaidi  
       
 
 
Web Mail
Mijadala
 
 
     
Hotuba za Mkuu wa Mkoa  
Hotuba za Katibu Tawala (M)  

 
 
 
 
   
       
 

 

  Mashirika, Taasisi & NGO's  
    ......................................................  
  Hoteli & Nyumba za kulala wageni  
    ......................................................  
  Hospitali, Vituo vya afya na zahanati  
       
  Huduma za Jamii  
    ........................................................  
© 2014 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa S.L.P 119 Mwanza, Simu:028-2501037/2500366,Fax: 0282501057;Email:info@mwanza.go.tz,ras.mwanza@pmoralg.go.tz